Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wamefanya kongamano la vijana katika kupinga rushwa na dawa za kulevya katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini Arusha.
akifungua Kongamano hilo, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Zawadi Ngailo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella.
Jumla ya washiriki 547 walihudhuria kongamano hilo; ikihusisha wanafunzi wa shule tisa za Sekondari kutoka Wilaya ya Arumeru na Jiji la Arusha, waraibu wanawake, na wadau wengine mbalimbali.