MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) maimuna Pathan amewaomba wananchi kuendelea kupata huduma kwenye hospitali za serikali kwa kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan ameboresha huduma za kiafya kwa zaidi ya asilimia 100.
Mbunge Maimuna alisema kuwa kila kona ya nchi ya Tanzania kimejengwa hospitali za wilaya ambazo zinatoa huduma kwa ubora unaotakiwa kama ambavyo swali zilikuwa zinatolewa kwenye hospitali za watu binafsi hivyo wananchi rudi kupata huduma ya afya kwenye hospitali za serikali.
Alisema kuwa kuanzia hospitali za wilaya na baadhi ya vituo vya afya nchi kuna madaktari bingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali ambayo swali kulikuwa hakuna huduma kama hizo.
Watanzania wenzangu twendeni tukapata huduma za kiafya kwenye hospitali za serikali, turudi nyumbani kumenoga mama Dr Samia suluhu Hassan anaupiga mwingi