Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha.
Ikiwa leo ni Machi 08,2024 kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, Mtaandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha wameunga na wanawake wengine Mkoani humo huku Mtandao huo wakiitumia siku hiyo kuwawekea akiba ya fedha katika mfuko wa uwekezaji (UTT) kwa Watoto wawili wa askari wanandoa waliofariki kwa ajali ya gari.
Akiongea katika Viwanja vya Ngarenaro Complex Jijini Arusha Mwenyekiti wa Mtandao huo Mkoa wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mtaandao huo katika kuelekea kilele hicho ulianza mapema kutoa elimu maeneo mbalimbali Pamoja na kufanya ibada ya kuwaombea marehemu.
SSP Zauda ameongeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo waliona vyema kuunga na kuwawekea akiba ya fedha kwa Watoto wa askari wanandoa waliofariki katika ajali ya gari ambapo amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia Watoto hao katika swala la elimu na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Aidha ametoa wito kwa wanawake wengine Mkoani humo kufanya kazi kwa bidii,nidhamu na kutenda haki ili ustawi bora na wajikwamue kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.
Nae mrakibu msaidizi wa Polisi Lucy Teesa kutoka Makao Makuu ya kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo STPU amewaomba wanaweka wenzake kushiriki vyema katika mapambano dhidi uhalifu ambapo amewaomba kutoa taarifa za uhalifu na kujikitaa katika malezi bora ya Watoto ili kujenga Jamii iliyostarabika.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Murieti Mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Tausi Mbalamwezi amewaomba wanawake wenzake kujiamini na kujituma katika kutekeleza majukumu yao huku akiwaomba kuumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliinua taifa kiuchumi.