Na Mwandishi wetu, Babati
WAFANYAKAZI wa shule ya awali na msingi ya Tarangire ya Mjini Babati Mkoani Manyara, washerehekea siku ya wanawake duniani kwa maandamano, bashasha na nderemo.
Wafanyakazi hao wakiongozwa na Makamu Mkuu wa shule bi Eva Mrutu wamezunguka katika mji wa Babati na Viunga vyake wakiimba wimbo ( I m a super woman). Mimi ni mwanamke shupavu.
Naye Mwalimu anaehusika na rasilimali watu katika tasisi hiyo Bi Mercy Randa amesema shule hiyo inaitambua siku hii inayoadhimishwa kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu. Ambapo mwaka huu imeadhimishwa tarehe 08.03. 2024 ikiwa na kauli mbiu “Wekeza kwa mwanamke,Kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii”
Amesema kauli mbiu hii imekuja katika wakati muafaka katika shule yetu ambapo wanafunzi wengi katika madarasa yao ni wasichana zaidi ya asilimia 65.
Pia amesema wafanyakazi zaidi ya nusu ni wanawake na zaidi ya 70% ya wanaolipa ada na kwa wakati ni wazazi kina mama.
“Menejimenti ya shule zaidi ya asilimia 80% ni kina mama vijana ambao sasa wameiva baada ya kufundishwa kwa takriban miaka 8 jinsi ya kusimamia mambo mbalimbali hususa kuwekeza kwa mtoto wa kike,” amesema.
Aidha Madam Mercy ameutaka umma wa watanzania kuchangamkia fursa za masomo zinazopatikana katika shule hiyo iliyoko Babati mjini, ya mchepuo wa kingereza, msingi na awali, kutwa na bweni, wasichana na wavulana.
Mawasiliano 0689539704, 0765012776,0752774514.