Aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ritha Mlaki (wa tatu kutoka kulia) akikata utepe wakati akizindua Akaunti Maalumu ya Tunu kwa ajili ya kuwasaidia ya Wanawake kiuchumi katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ritha Mlaki akizungumza jambo katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyokwenda pamoja na Uzinduzi wa Akaunti Maalumu ya Tunu katika hafla iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki Dkt. Ibrahimu Mwangalaba akizungumza jambo katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyokwenda pamoja na Uzinduzi wa Akaunti Maalamu ya Tunu katika hafla iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mahusiano Maendeleo Benki Magreth Msangi akizungumza jambo katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyokwenda pamoja na Uzinduzi wa Akaunti Maalamu ya Tunu kwa ajili kuwasaidia Wanawake katika hafla iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Joyce Mapunjo akizungumza jambo katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyokwenda pamoja na Uzinduzi wa Akaunti Maalamu ya Tunu kwa ajili kuwasaidia Wanawake katika hafla iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media Nengida Johanes (katikati) akichangia mada katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyokwenda pamoja na Uzinduzi wa Akaunti Maalamu ya Tunu kwa ajili kuwasaidia Wanawake katika hafla iliyofanyika leo Machi 8, 2024 Jijini Dar es Salaam.
…..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Maendeleo Benki imezindua Akaunti Maalumu ya Tunu yenye lengo la kuwasaidia Wanawake kiuchumi ili waweze kutimiza ndoto zao jambo ambalo litasaidia Taifa kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za Maendeleo.
Akizungumza leo tarehe 8/3/2024 jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Akaunti ya Tunu, aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ritha Mlaki, amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupigania nafasi ya mwanamke ukilinganisha na miaka ya nyuma, huku akiwataka wanawake nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na akaunti Tunu kujiletea maendeleo.
Mhe. Mlaki amesema kuwa serikali ya Tanzania imejitaidi kuweka sera na sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya ardhi inayotoa fursa kwa mwanamke kumiliki ardhi.
“Tunaishukuru Benki ya Maendeleo kwa kuanzisha Tunu akaunti kwa ajili ya wanawake ambayo inakwenda kuwasaidia na kutoa fursa mbalimbali za maendeleo” amesema Mhe. Mlaki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki Dkt. Ibrahimu Mwangalaba amesisitiza umuhimu wa wanawake kutumia akaunti ya tunu ili waweze kuongeza kipato chao.
Dkt. Mwangalaba amesema kuwa benki ya maendeleo imewekeza kwa wanawake ili kuhakikisha wanaongeza kipato kupitia biashara na shughuli za kiuchumi ambazo ni nguzo na uhai kwa Taifa.
“Uchumi ukiwa imara nchi inapata kodi na kufanikiwa kujiendesha bila shida yoyote, wakinamama unapambana katika hili na ili mpige hatua benki imeona iwapatie akaunti ya tunu ambayo inakwenda kupandisha kipato chako” amesema Dkt. Mwangalaba.
Dkt. Mwangalaba amewataka wakinamama kuwa na nidhamu, kufanya kazi kwa bidii katika utendaji kazi ili kuongeza ustawi katika jamii na taasisi mbalimbali.
Meneja wa Mahusiano Maendeleo Benki Magreth Msangi, amesema kuwa akaunti ya tunu ni maalumu kwa ajili ya mwanamke yoyote mwenye miaka kuanzia 18 na kuendelea.
Msangi amesema kuwa utaratibu wa kufunga akaunti ya tunu mwanamke anatakiwa kuwa na picha moja, kitambulisho cha NIDA pamoja na shillingi elfu kumi kwa ajili ya kufungulia.
“Akaunti ya Tunu inakusaidia kuweka fedha kila siku na kadri unavyoongeza fedha katika akaunti na riba inaongezeka, pia hakuna makato ya kila siku” amesema Msangi.
Amesema kuwa kupitia akaunti ya tunu itawasaidia kuwa kikundi cha wanawake ambacho watakuwa wanapewa mafunzo kwa ajili ya kukuza biashara zao pamoja na kupata elimu ya kifedha.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.