……….
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, wanawake na Makundi maalumu Dk. Dorothy Gwajima amewaasa wanawake wakuu wa Taasisi mashirikia na vyuo vya umma nchini kuanzisha na kuunga jitihada za programu za kukuwainua wanawake Kiuchumi katika shughuli mbalimbali za Kiuchumi katika ngazi za Mamlaka wanazosimamia.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyowakutanisha iliyowakutanisha wanawake wakuu wa mashirika,Taasisi na wanasiasa wanawake wakongwe.
Amesema kupitia dhana ya usawa wa kijinsia katika sekta zote ikiwemo ya uongozi itasaidia kuwainua wanawake waliokata tamaa kuzungumza kwa vitendo na kusimama imara.
” Tutakaposimamisha uongozi katika ngazi zote tutaweza kunusuru mambo ambayo yamekuwa chagamoto katika jamii kwani wanawake ni zaidi ya asilimia 51 huku duniani. Kusimama kwa wanawake katika nafasi mbalimbali haimaanishi kushindana na wanaume bali ni kila mmoja kutimiza majukumu yake yanayomuhusu,” amesema
Aidha Gwajima amewataka wanawake hao kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kila hatua anayoifanya katika kuleta Maendeleo kwa watanzania na kusaidia uwepo wa usawa wa Jinsia .
Kwa upande wake Mgeni Maalum katika tukio hilo,Balozi Amina Salum Ali amewataka wanawake wenye nafasi za juu kuwasaidia wenye nafasi za juu kuwasaidia kwa mawazo ya hali na Mali kwa wanawake wanaowaongoza badala ya kutumia nafasi kuwakandamiza.
“Niwaombe wanawake viongozi kuhakikisha mnawasaidia wanawake wenzenu waliopo chini katika kuwaongoza na sio kuwakandamiza kwa kutumia nafasi zenu,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (Tantrade) Latifa Mohamed Hamis amesema wameamua kuungana pamoja kwa lengo la kubadilishana uzoefu, na kuutumia kwa ajili ya kujipanga na kutathimini masuala mbalimbali .
“Siku hii muhimu kwetu sisi kama wanawake viongozi wa Taasisi za umma kuwa sehemu ya sherehe zetu kukutana na kujitathimini pamoja na kubadilishana mawazo yetu yatayoweza kusaidia jamii zetu tunazoziongoza,” amesema Latifa.
Amefafanua kuwa, kwa mara ya kwanza wanawake viongozi wa Taasisi za umma wameamua kukusanyika pamoja, na kueleza kuwa mikutano hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha majumuiko hayo yanaleta faida katika jamii wanazoziogoza.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa usimamizi wa hakimiliki kutoka Ofisi ya hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare amesema umoja huo upo katika malengo tofauti ikiwemo ya kujisajili ili kuhakikisha unatimiza malengo ambayo umejiwekea.
Sinare alisema Umoja huo unaundwa na kamati ya mpito ambayo inahususisha viongozi wa Taasisi za umma.
Aidha Jukwaa hilo lilitoa tuzo kwa maalumu kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama ishara ya kumuunga mkono na kumpogeza kwa kazi ambazo amekuwa akiizifanya
Tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Dkt Samia ilipokelewa na Waziri Gwajima ambapo mbali na tuzo hiyo pia wametoa tuzo kwa wakuu wa Taasisi mwanamke katika nafasi zao kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanatimiza malengo ya kitaasisi na yaliyowekwa na nchi.