Na Sophia Kingimali
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema mtaala mpya wa mafunzo ulioanza kutumika mwaka huu utasaidia watoto kujifunza kwa vitendo ambapo mtoto anapotoka shule anakuwa na uwezo wa kujiajiri au kuajiliwa.
Hayo ameyasema leo March 7,2024 jijini Dar es salaam kwenye kikao cha mafunzo ya mataala mpya kwa wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali ya habari nchini lengo likiwa kuwajengea uelewa kuhusu mtaalam mpya ili waweze kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vyao vya habari.
Amesema mtaala huo umeanza kwa shule za awali,darasa la kwanza na la tatu ambapo shule ya awali mtoto atasoma kwa mwaka mmoja na kuingia darasa la kwanza ambapo atahitimu darasa la sita na kulazimika kusoma mpaka kidato cha nne kwa amri.(lazima)
“Mtaala huu unamtaka mtoto kusoma kwa miaka 10 kwa lazima ni lazima mtoto amalize kidato cha nne kwa amri”amesema.
Aidha amesema kuwa katika mtaala huo mtoto atasoma masoma ya amali na kawaida yaani mtoto atachagua ambapo mafunzo ya amali mtoto akimaliza shule anaweza kujiajili.
Aidha ameongeza kuwa katika mtaala huo mpya umeeleza mtoto kufundishwa somo la ujasiliamali hivyo walimu wa somo hilo wanaandaliwa ambapo sasa wameanza kwa mkondo wa elimu ya amali pekee.
“Kwa watoto watakaosoma amali watakapoenda elimu ya juu watasoma miaka mitatu na wakimaliza watapata cheti cha kuhitimu lakini pia cheti cha Veta”,Amesema.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Caloryne Nombo amesema utekelezaji wa mtaala huo unaenda sawa maboresho ya sera ya elimu.
Amesema utekelizaji wa sera hiyo ulikua shirikishi kama maagizo yalivyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka sera hiyo ipitiwe kwa miaka miwili huku ikishirikisha majadiliano ya wadau mbalimbali.
“Tumefanya majadiliano na jamii ya kitanzania kuhusu sera hiyo na baadae ikaidhinishwa na baraza la mawaziri hivyo tunawaomba wanahabari mtusaidie kutoa elimu ya mtaala mpya kwa jamii kwani tumaamini mnanguvu kubwa ya ushawishi katika kuifikia jamii”Amesema Prof Nombo.
Sera ya elimu imejikita katika katika maeneo 7 ambayo ni Mfumo wa elimu na mafunzo,fursa za elimu,ubora wa elimu na mafunzo,Rasilimali watu,usimamizi na uendeshaji,mfumo wa ugharamiaji na masuala mtambuka.
Aidha mtaala huo utazingatia kulea na kuendeleza vipaji na vipawa katika mfumo wa elimu.