Wekundu wa Msimbazi Simba SC imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prison katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania uliopigwa leo Machi 6, 2024 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Simba Sc walikuwa wenyeji wa mchezo huo ambapo Tanzania Prison walifanikiwa kupata matokeo kupitia mshambuliaji Samson Baraka Mbandhigula dakika ya 45, na 62, huku bao pekee la Simba likifungwa na kiungo Mkongo, Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 89.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 27 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya nne, wakati Simba SC inabaki na pointi zake 36 za mechi 16 sasa nafasi ya tatu.