Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Said Shaib Mussa ameendelea kuongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha
Kamati ya Fedha ya Jumuiyai ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika (SADC)
kinachofanyika Jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.
Pamoja na masuala mengine, kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa ya Kamati
Ndogo ya Fedha ya SADC na Kamati ya Ukaguzi ambapo ajenda mbalimbali zimejadiliwa
ikiwemo mpango wa bajeti ya kanda kwa kipindi cha 2024/2025 na mapendekezo yake
yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuidhinishwa tarehe 10 na
11 Machi, 2024.
|
|
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw, Rished Bade, Afisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Joseph Haule na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Noah Mboma wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Fedha cha SADC kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024. |
|
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifuatilia majadiliano ya Kikao cha Kamati ya Fedha kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024. |
|
Balozi Mussa akiteta jambo na sehemu ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Tanzania na Afrika Kusini. |