Na Sophia Kingimali
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Furahika amewataka wazazi na walezi kuacha kukaa na watoto waliomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na elimu ya juu kuwapeleka kwenye vyuo vya ufundi stadi ili kuepuka ongezeko la vijana mtaani wanaojihusisha na matukio ya kiarifu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo March 5,2024 jijini Dar es salaam wakati akitangaza kozi mpya ya Water mita(wasoma mita za maji) mkuu wa chuo hicho David Msuya amesema wametaendelea kuwasaidia vijana kuweza kutomiza malengo yao.
Amesema kozi hiyo itatolewa bure kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ambapo mzazi atachangia kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia.
Sambamba na hayo Msuya ametangaza nafasi za kazi za udereva kwa madereva wastaafu wenye umri wa miaka 60 na kuendelea ambae anaweza kuendesha gar ya manyo lengo likiwa kutumia busara na uzoefu wao wa kazi lakini pia kuwatoa nyumbani wazee hao nakuwatumia katika shughuli ndogondogo.
“Tumelenga wazee kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuendelea kutumia kuwatumia na kutumia busara zao katika kuwafundisha wanafunzi lakini pia kutoa ushauri wao pindi unapohitajika sisi kama chuo tumewalenga hao na si hao tu hata wale waliofanya kazi za udereva na kuachishwa kwa sababu mbalimbali lakini ana umri huo pia tunawapokea”,Amesema Msuya.
Sambamba na hayo pia wametangaza nafasi za kazi kwa walimu wa kike wa kozi ya hotel ambae amesoma ngazi ya shahada na Astashahada lakini pia walimu wa kujitolea kwenye kozi nyingine ambazo zinatolewa chuoni hapo pia wanahitajika.
Chuo cha ufundi stadi Furahika chenye namba za usajili VET/DSM/PR/2021/D169 kinaendelea kupokea wanafunzi katika kozi mbalimbali ikiwemo ushonaji,Hotel,Bandari,fundi bomba,udereva na nyingine nyingi bila malipo ambapo mwanafunzi atajigharamia vifaa tu.