MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Lindi kupitia chama Cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amekabidhi zaidi ya mashuka 100 katika hospitali za wilaya Mkoa wa Lindi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashuka hao katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea Mbunge Maimuna Pathan alisema kuwa amenunua na kutoa mashuka hayo kwa lengo la kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya.
Pathan alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan imefanya mambo mengi na makubwa katika kuboresha sekta ya afya hivyo ni muhimu wananchi na viongozi kumuunga mkono Rais Dr Samia.
Alisema kuwa ataendelea kununua mashuka mengine zaidi hayo na kuyapeleka kwenye hospital,zahati na vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi.
Pathan alisema kuwa sekta ya afya imeboreshwa sana katika awamu hii ya sita hivyo sasa hakuna haja ya wananchi kwenda kupata huduma nje ya hospital za serikali kwa na madaktari bingwa Kila hospital za wilaya, Mkoa na taifa Kwa ujumla
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini Tanzania.