Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
…………………….
Chanzo Best Media
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameweka wazi kwamba sasa anaondoka ndani ya uongozi wa chama hicho bila huku akiicha kama taasisi ambayo haitegemei kujengwa kwa majina ya watu.
Hayo ameyasema leo Machi 4, 2024 katika mahojiano maalumu yaliyorushwa kituo cha redio cha Clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast, ambapo amesema kuwa ACT Wazalndo, kimeweka utaratibu wa kubadilishana uongozi ambapo kupitia utaratibu huo wanaamini kutaimarisha demokrasia na kuwa na taasisi imara nyakati zote.
“Sisi kama ACT Wazalendo tumeweka utaratibu wa kubadilishana uongozi na tunaamini kwamba mkiweka huo utaratibu chama kitaweza kuimarika kitaasisi, chama hakitatambulika kwa mtu, nyinyi mnafahamu kwamba sasa hivi ukienda mtaani mtaambiwa kwamba bila Zitto Kabwe hakuna ACT Wazalendo.
“Na tulikuwa tunaambiwa kwamba Maalim Seif Sharif Hamad (aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais SMZ) amefariki na ACT Wazalendo imekufa na haitakuwepo lakini tumeweza kuwepo na tumeendelea kukua kwa kasi zaidi,” amesema Zitto
Kutokana na hali hiyo amesema kuwa anaondoak kwenye uongozi wa chama na chama hicho kinapaswa kuendelea kuwepo kwani yeye na wenzake muda wote walijitahidi kukitengeneza kama taasisi ambayo ni zaidi ya mtu mmoja.
“Sasa hivi Zitto Kabwe anatoka kwenye uongozi na chama kinapaswa kuendelea kuwepo, sisi tunajitahidi kutengeneza taasisi ambayo ni zaidi ya mtu mmoja, sasa inawezekana kwamba vyama vingine wao hawaoni kama ni jambo ambalo lina manufaa kwao, kwa hiyo ni vigumu sana mimi (Zitto Kabwe) ambaye ni kiongozi wa chama kingine kutoa maoni kuhusiana na taratibu za vyama vingine na ukitaka hayo maoni inabidi uwaite na uwaulize wao,” amesema
Zitto ambaye amewahi kuwa Mbunge katika majimb ya Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini kwa nyakati tofauti, amesema kuwa hata hatua ya chama hicho kufikia kuwa na midahalo kwa wagombe wake wa nafasi mbalimbali kama njia ya kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama hico na inaonesha ni tofauti na Chama tawala CCM ambao alidai hukwepa midahalo.
“Leo tutakuwa na midahalo ya wagombea wa nafasi zote za juu na tunafanya hivi kwa sababu huku nje nyakati za chaguzi kubwa tunalalamikia kwamba CCM wanakimbia midahalo, hawataki midahalo na sisi tunataka tukutane nao kwenye midahalo, huku ndani lazima na nyie muonyeshe mnayaishi hayo?.
“Yaani muwe mfano, tumeamua kujenga taasisi yetu (ACT Wazalendo) kwa misingi ile ambayo tunaipigania nje, tuipiganie na ndani. Huwezi kusema watu wanakaa madarakani muda mrefu lakini wengine ila sio wewe, au kusema kwamba hamna demokrasia lakini ndani wewe huangalii demokrasia, nje ndio unaangalia demokrasia, tumesema hapana tunataka tujenge demokrasia kwa mujibu vile ambavyo tunataka na ndio haya ambayo mnayashuhudia ndani ya ACT Wazalendo katika kipindi hiki cha wiki nzima,”