Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Bw. Ricky Pascal na Bi. Twidike Ntwima wakibandika fomu za utezi wa wagombea wa udiwani Kata ya Kimbiji leo baada ya muda wa uteuzi kumalika Saa 10:00 jioni ya Machi 4,2024. Wagombea 14 waliochukua fomu wameteuliwa kuwania nafasi hiyo.
Wagombea wa Udiwani Kata ya Kimbiji wakitazama fomu za uteuzi zilizobandikwa katika ubao wa Matangazo katika Ofisi za Kata ya Kimbiji. Wagombea 14 waliochukua fomu wameteuliwa kuwania nafasi hiyo.
Wagombea wa Udiwani Kata ya Kimbiji wakitazama fomu za uteuzi zilizobandikwa katika ubao wa Matangazo katika Ofisi za Kata ya Kimbiji. Wagombea 14 waliochukua fomu wameteuliwa kuwania nafasi hiyo.
Wagombea wakikabidhiwa fomu zao za uteuzi baada ya Tume kuwateua kuwa wagombea udiwani Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dares Salaam wamerejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi Mfogo wa udiwani uyakaofanyika Machi 20,2024.
Wagombea wakikabidhiwa fomu zao za uteuzi baada ya Tume kuwateua kuwa wagombea udiwani Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dares Salaam wamerejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi Mfogo wa udiwani uyakaofanyika Machi 20,2024.
Na Mwandishi Wetu, Kigamboni
Wagombea 14 waliochukua fomu za utezi kuwania udiwani Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dares Salaam wamerejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi Mfogo wa udiwani uyakaofanyika Machi 20,2024.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Bw.Ricky Pascal alisema wagombea hao walianza kuchukua fomu za uteuzi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyopanga Februari 27,2024 hadi leo Machi 4,2024 na wote kukamilisha ujazaji fomu na kuzirejesha.
Wengine ni Bw. Michael Makile Mzalendo (UDP), Joyce Ephraimu Mweigule (DP),Bi. Janeth Pius Mhando (TLP),Nasra Twalib Kimo,Bw. Innocent Fratern Shirima (CCK), Neema Kassimu Yegeyege (UMD) na Juma Hassan Abdalah (NCCR-Mageuzi.
Wagombea hao walikabidhiwa fomu zao za uteuzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Bw. Ricky Pascal na Bi. Twidike Ntwima.
Tume ilitangaza uchaguzi Mdogo katika Kata 23 za Tanzania bara kufanyika Machi 20,2024 na fomu za uteuzi zilianza kutolewa Februari 27 hadi Machi 4 mwaka huu.
Mbali na Kata Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kata zingine zinazofanya uchaguzi ni Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).
Nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).