Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Mhe. Fuad Hussein katika moja ya kumbi za Mikutano za Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Nest wakati Mkutano wa Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya leo tarehe 3 Machi, 2024, Jijini Antalya Uturuki.
…………………
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Mhe. Fuad Hussein katika moja ya kumbi za mikutano za Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Nest wakati Mkutano wa Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya leo tarehe 3 Machi, 2024, Jijini Antalya Uturuki.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuendeleza mahusiano ya karibu kati ya Serikali ya Tanzania na Iraq pamoja na Mabunge ya nchi hizo mbili kushirikiana katika nyanja za kidiplosia za kibunge.
Aidha, wamejadili namna ya kuendelea kuchagiza amani na usalama kwa njia za kidiplomasia katika eneo la Mashariki ya kati na kuitumia Iraq kama nchi ya mfano wa kuigwa kutokana na historia yake na namna ilivyoweza kujikomboa na kuwa taifa huru lenye kujenga na kufuata misingi imara ya kidemokrasia.