Askari wa Jeshi la Uhifadhi (JU) nchini wametakiwa kuzingatia uwadilifu na misingi ya Jeshi hilo ili malengo ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Jeshi hilo yaweze kufikiwa na kwa askari yeyeto atakaekiuka taratibu, kanuni na sheria hatua kali zitachukukiwa dhidi yake.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba Wilayani Biharamuro Mkoani Kagera, alipokuwa akizungumza na uongozi wa Hifadhi ya Taifa Chato, na askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).
CP Wakulyamba licha ya kuwapongeza askari hao kwa kazi nzuri wanazofanya, amesisitiza kuwa, uongozi wa Wizara hiyo hautoa mvumilia askari askari yeyote atakae kwamisha jitihada za Wizara za usingizi bora wa Uhifadhi hususani katika kupambana na ujangili, mifugo ndani ya Hifadhi na Uchomaji moto Misitu iliyohifadhiwa kisheria.
Awali akitoa Taarifa za ya utekelezaji wa majukumu ya Hifadhi ya Burigi Chato, Mkuu wa Hifadhi Burigi Chato, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Ismail Omari Ismail, amesema ndani ya muda mfupi wa uongozi wake wamefaniliwa kupamba na uingizaji wa mifugo ndani ya Hifadhi kwa asilimia 225 kutoka Januari 2022 – February 2023 mifugo 13,839 hadi 6, 154 kwa Januari 2023 – Februari 2024 na kuwa zoezi hili ni lakudumu.
Aidha Ismail kwa niaba ya watumishi wengine ameahidi kufanyia kazi maagizo yote waliopewa na uongozi wa Wizara hususani kusimamia nidhani ya askari, kubuni njia mbalimbali za kiuchumi na kuimarisha mahusiano mema, na viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa hadi Vijiji pamoja na wanchini waishio pambezoni mwa Hifadhi.
Katika hatua nyingine CP Wakulyamba amekutana na Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Biharamuro na kuupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa ushirikiano unaotoa katika uhifadhi wa Hifadhi ya Burigi Chato, na kuahidi kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Angellah Kairuki itaendelea kushirikiana vyema na uongozi wa Wilaya hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro SACP. Advera Bulimba amesema, hapendezwi kuona baadhi ya watu wanafanya shughuli za kijamii ndani ya Hifadhi kama vile kilimo, uchomaji wa Mkaa na ufugaji hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama chini yake itaendelea kushirikiana na Wizara ili kutokomeza changamoto hiyo ili Hifadhi hiyo iendelee kuwa neema kwa wanachi wa Biharamuro na Tanzania kwa ujumla.