Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dk. Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni mmoja wa watoto wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili Hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole mmoja wa Wajane wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Bi Siti Mwinyi (aliyekaa), baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, shughuli iliyofanyika Jumamosi, Machi 2, 2024, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiweka mchanga kwenye kaburi, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, aliyezikwa leo Jumamosi, Machi 2, 2024, huko Mangapwani, Mko wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.