Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Ujumbe wa Taasisi ya Nafaka ya Msumbiji (ICM) uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Alfredo da Piedade João Nampuio, tarehe 29 Februari, 2024.
Ujumbe huo ulifika katika Ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha na kuwasilisha ombi la kutaka kuanzisha Ushirikiano kati yake na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) nchini Tanzania. Pamoja na mambo mengine, ushirikiano huo utawezesha upatikanaji wa soko la mahindi nchini Msumbiji.