Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasili katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam katika shughuli ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo Machi 1, 2024..
………
Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya Jamhuri Muungano wa Tanzania Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi ukiwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya viongozi wa Serikali na wananchi kutoa heshima ya mwisho leo Machi 1, 2024 .
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaongoza shughuli ya kuaga mwili wa hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Taifa kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu.
Baadhi ya wananchi waliofika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuaga Mwili wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wamesema kuwa watamkumbuka kwa mambo mengi ikiwemo kama mwasisi wa Demokrasia ya vyama vingi nchini.
Mkazi wa Manispaa ya Temeke Bw. Emmanuel John amesema kuwa akiwa kiongozi hayati Mwinyi alikuwa msikivu na mtulivu katika utekelezaji wa majukumu yake
“Tutamkumbuka kwa falsafa yake ya Ruska kwa kuruhusu bidhaa nyingi kuingia nchini ili kumaliza changamoto zilizopo kwa wakati huo” amesema Bw. John.
Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi
amefariki dunia February 29, 2024 katika Hospital ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na tayari Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani ametangaza siku saba za maombolezo kuanza leo Machi 1, 2024.
Atazikwa Machi 2, 2024 Nyumbani kwake huku Mwangapwani Zanzibar, baada ya viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi kutoa heshima za mwisho