Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) mkoa wa Mara Mhandisi Vedatus Maribe kuhusu maendeleo ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Musoma mkoani Mara, ambao utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 35, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuashiria awekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Maige Gibai wakati ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri hiyo, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
DSC_1674 DSC_1709 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Maige Gibai wakati akifanya ukaguzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri hiyo, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, katika uwanja wa Bwai Paris mkoani Mara, Februari 29, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Februari 29, 2024 ameweka jiwe la msingi la jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma katika kata ya Suguti ambalo hadi sasa limegharimu sh. bilioni 2.48 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala, uzio na ununuzi wa samani za ofisi.
Mara baada ya kuweka jiwe la msingi, Waziri Mkuu alikutana na watumishi na madiwani wa Halmashauri hiyo na kuwasisitiza watambue kuwa wameletwa hapo Saguti ili wawatumikie wana-Musoma Vijijini.
“Jukumu lako mtumishi ni kutumia elimu yako na ubunifu wako ili kuwahudumia wananchi hawa. Wekeni mipango kazi ya robo mwaka, nusu mwaka na ya mwaka. Tunataka tuone hiyo mipango ikitoa matokeo,” amesisitiza.
Pia amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kuepuka mtandao wa wizi kama ilivyofanyika kwenye baadhi ya Halmashaur za mkoa huo.
Amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Msongela Palela awasiliane na taasisi za NHC na Watumishi Housing ili waende kujenga nyumba za watumishi kwenye Halmashauri hiyo kwa mkataba maalum.
“Mara ya mwisho niliagiza kuwa watumishi wahame kutoka mjini waje wakae huku. Tunataka watumishi wakae karibu na ofisi zao, badala ya kutoka mjini,” amesisitiza.
Pia alimwagiza ashirikiane na Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, ili wakamilishe ujenzi wa vituo vya afya vitano ili vianze kutoa huduma kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Maige Gibai amesema ujenzi wake utasaidia kusogeza karibu huduma karibu na wananchi ambapo awali walikuwa wanasafiri takribani kilomita 90 kwenda Musoma mjini.
Pia, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuidhinisha fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo na wananchi ambao walitoa bure eneo la ujenzi lenye ukubwa wa ekari 200.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake katika Manispaa ya Musoma ambako atazungumza na wananchi katika uwanja wa Mara Sekondari.