Wananchi wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuhakikisha wanazingatia usafi na kula vyakula vya moto na salama
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi aliyoifanya katika viwanja vya Ilalila senta ambapo amesema kuwa wilaya ya Ilemela inakabiliwa na ugonjwa wa Kipindupindu hasa maeneo ya pembezoni mwa ziwa Viktoria hivyo kuwataka wananchi kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo
‘.. Natambua kuwa wilaya yetu inakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu, Sasa tusipoambiana tukaanza kuchukua hatua za kujilinda tutaathirika wengi ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa utekelezaji wa maendeleo ndani ya Jimbo lake ambapo miradi mikubwa na ya kimkakati imeweza kutekelezwa huku akiwataka wananchi kukiamini CCM na kuwachagua viongozi wake katika uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za mitaa
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Hasan Milanga amesema kuwa wanajivunia kazi nzuri zinazofanywa na wawakilishi wa chama chake hasa Rais Dkt Samia, Mbunge Dkt Angeline, diwani na wenyeviti wa mitaa na kwamba chama hicho kitashinda katika uchaguzi mkuu unaokuja Kwa kuwa wametekeleza ilani ya uchaguzi Kwa kiwango kikubwa
Naye diwani wa kata ya Shibula Ndugu Swila Dede mbali na kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Kwa kazi nzuri zinazofanyika ndani ya kata yake amewataka viongozi kushirikiana katika kutatua kero za wananchi
Steven Paul ni mwananchi wa kata ya Shibula ambapo amepongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Samia kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuwataka wananchi wenzake kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo
Katika hatua nyengine Dkt Angeline Mabula amempokea aliyekuwa mwaachama na kada wa chama cha upinzania CHADEMA baada ya kuridhishwa na kazi ya utekelezaji wa maendeleo