Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari Kando ya mkutano wa majadiliano wa ngazi ya juu kuhusu muelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 wa kuongeza kasi ya uchumi himilivu na maendeleo Jumuishi uliofanyika kwenye ukumbi wa BoT Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo, Mhe. Balozi David Concar, ambaye pia ni Balozi wa Uingereza nchini, akizungumza wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT, jijini Dar es Salaam.
…………………
NA JOHN BUKUKU DAR ES SALAAM
Wadau wa maendeleo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.
Hayo yamebainishwa Leo Feburuari 29, 2024 na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza Kando ya mkutano wa majadiliano wa ngazi ya juu 2024 kuhusu mwelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 wa kuongeza kasi ya uchumi himilivu na maendeleo Jumuishi uliofanyika kwenye ukumbi wa BoT Jijini Dar es salaam.
Amesema wanapojiandaa na dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kazi endelevu inayofanywa na Rais Dkt. Samia ya kukuza uchumi jumuishi ambao haumuachi mtanzania nyuma na uwekezaji anaoufanya ni ule unaolenga sekta za uzalishaji ambazo zina ajili zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.
“Hata katika kipindi cha misukosuko ya kiuchumi duniani baada ya Uviko 19,mizozo ya Rasia na Ukraine pamoja na uhaba wa fedha za kigeni lakini inchi yetu bado imeweza kuwa na ustahimilivu kwenye vigezo vyote vya uchumi”, amesema Dkt. Nhemba
Ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza kuna miradi mikubwa ya umwagiliaji mpaka vijijini ambapo kunavijiji viliwahi kupata Bilioni 30 kwaajili ya wakulima,Rais Samia anafanya yote hayo kwaustawi wa watanzania.
Akizungumza suala la ugumu wa maisha Dkt. Nchemba amesema wanaangalia uwekezaji mkubwa unaoelekezwa kwenye shughuli za uzalishaji kwasababu huo unaenda kupunguza pengo la walionacho na wasionacho.
“Uwekezaji unaolenga kwenye Sekta zinazoajili watu zaidi ndio unaenda kutoa jawabu la kudumu kwenye ustawi wa watanzania”, amesema
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa REPOA Donald Mmari amesema majadiliano hayo yanayofanyika kila mwaka yanaumuhimu kwani yanawaleta pamoja wadau wa maendeleo, Serikali,wahisani na taasisi za utafiti kujadiliana kwenye maeneo ya muhimu ili kuhakikisha uchumi unaendelea kukua.
Ameeleza kuwa wako kwenye hatua ya kufanya tathimini ya walikotoka katika utekelezaji wa dira ya Maendeleo ya miaka 25 na wanakwenda kuandaa dira ya mwaka 2050.
“Wahisani wanaweza kuwekeza nguvu zao wapi katika kuhakikisha vipaumbele vya nchi vinatekelezwa na malengo ya kukuza uchumi kutokomeza umasiki yanafanikiwa kwa asilimia 100”, amesema.
Aidha, ameeleza watanzania wengi wanahitaji ajira na kumekuwa na ugumu wa upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana kutokana na uwekezaji mdogo hivyo uwekezaji unatakiwa uwe mkubwa zaidi hatua itakayosaidia kuondokana na changamoto ya ajira.
Sekta binafsi inahitaji mazingira ya biashara ambayo ni rafiki pia upatikanaji wa nishati, huduma za uchukuzi ambazo zinaweza kufanya biashara zao kuwa shindani ili waweze kuongeza wigo wa ajira nchini.