Na John Walter -Manyara
Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kila mkoa kujenga ofisi za wafanyabiashara wadogo (Machinga) limetekelezwa mkoani Manyara.
Akiwahutubia Wananchi wa mkoa wa Geita Oktoba 15,2022, Rais Samia aliwaagiza wakuu wa mikoa Kote nchini kutenga maeneo rafiki ambayo Machinga watapewa bure kwa ajili ya kujenga ofisi hizo ambapo alitoa Shilingi milioni kumi kila mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga leo tarehe 27, 2024 amezindua Ofisi ya Shirikisho la Wamachinga na Bodaboda iliyojengwa mjini Babati.
Ofisi hiyo imejengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43, ikiwa na umeme, maji pamoja na samani ambapo fedha hizo ni kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na michango ya wadau mbalimbali.
Sendiga ameahidi kununua Kompyuta mbili katika ofisi hiyo ili kuwawezesha kufanya Biashara zao kidijitali.