Mkuu wa INTERPOL Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi DCP: GEMINI SEBASTIAN MUSHY kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma mapema leo tarehe Februari 25, 2024 alipanda mti eneo la mbele la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe baada ya kumaliza ukaguzi wa siku 07 ulioanza mnamo Februari 18 mwaka huu.
Naibu Kamishna MUSHY alifanya ukaguzi na kutoa mafunzo katika wilaya zote 04 za mkoa wa Songwe ambapo pamoja na kukagua kazi mbalimbali za Polisi Mkoani humo, pia amefanya vikao kwa nyakati tofauti tofauti na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali.
Aidha katika kikao chake cha majumuisho alichofanyika tarehe 25 Februari 2024 amewapongeza Maofisa, wakaguzi na Askari kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha usalama unaendelea kuimarika mkoani hapa hasa katika kuzuia vitendo vya uhalifu.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP. THEOPISTA MALLYA amemshukuru DCP. MUSHY na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuongeza imani yao kwa jeshi la Polisi.
Ukaguzi huo ni rasmi kwa mujibu wa Amri za kudumu za Jeshi la Polisi Tanzania.