NA DENIS MLOWE, IRINGA
JAMII imeshauriwa kutoangalia gharama za elimu pindi wanapotaka ubora na ufahamu mkubwa kwa watoto wao wanapotaka kuwapeleka shule.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi mzalishaji wa Kampuni ya Asas ,Ahmed Salim wakati wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa shule ya kimataifa ya Iringa (IST) wakati akizungumza katika mahojiano maalum na wanahabari
Ahmed Alisema kuwa wazazi au walezi wanatakiwa kuangalia zaidi ubora wa elimu ambao unatolewa na shule kwani gharama sio kitu endapo mtoto atapata elimu ambayo itamletea manufaa zaidi katika maisha yake.
Akitolea mfano yeye alisoma shule ya Iringa International na alifanikiwa kujiunga na chuo nchini Uingereza na kupata uwezo mkubwa na mafanikio katika maisha kwa kuwa shule Bora huzalisha wanafunzi Bora ambao ufahamu wao unakuwa mkubwa.
Alisema kuwa Kuna nadharia kwa baadhi ya watu shule Fulani ni Kwa ajili ya watu Fulani matajiri lakini kumbe sio hivyo kwani IST gharama zao ni nafuu ukilinganisha na ubora wa elimu wanaotoa kwa wanafunzi na ukiangalia wametoa asilimia 50 ya ada kwa wanafunzi wapya.
“kusoma shule kama hii inakupa exposure ya vitu vingi sana ikiwemo kukutana na watu wa mataifa mbalimbali na walimu kutoka nchi mbalimbali tunasema ubora wa elimu wa shule hii unaingia katika nchi yoyote” Alisema
Ahmed Salim Abri Alisema wazazi waondokane na hofu ikiwezekana wafike kuuliza tu aina ya wanafunzi waliotokana na shule hiyo kwa kuwa imekuwa ikitoa upana mkubwa kwa wanafunzi kujieleza na kukuza upeo wa kujua mambo na kujieleza popote pale.
Aliongeza kuwa gharama za uendeshaji wa shule ni kubwa kwa Sasa na utofauti wa masomo unakuja kutokana na aina ya mtaala ambao unatolewa shuleni Hapo wa Uingereza kufanya wanafunzi kuwa Bora sana katika vyuo mbalimbali pindi wakihitimu shuleni hapo.
Alitoa wito kwa wazazi kupeleka watoto shuleni hapo kwani Kuna faida kubwa kuliko gharama ambazo wengi wanahofu nazo na Kwa shule hiyo kwani wametoa punguzo na wasipate wasiwasi wa punguzo la ada kwa kudhani ubora wa elimu umepungua walete watoto wao kwa faida ya mbeleni.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa shule ya kimataifa ya Iringa, Majjid Mjengwa Alisema kuwa wamekuja na ofa ya punguzo la ada kwa asilimia 50 ili wanafunzi wengi waweze kujiunga hii katika kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Mjengwa ambaye pia ni mwalimu alisema kuwa watoto wake wote walisoma kwenye shule hiyo ni kutokana na ubora wa shule hiyo na kusema mawili makubwa ni utoaji wa ubora wa elimu yakiambatana na mazingira yake ambayo yana malezi mazuri.
Aidha alisema elimu shirikishi kwa wanafunzi wa shule hiyo na mataifa mengine yanafanya kuleta utofauti wa elimu katika shule hiyo ya kimataifa ya Iringa.
Alisema kuwa kwa kuangalia vitu hivyo aliweza kujinyima na kubana matumizi kwa Lengo la kuwapatia elimu Bora watoto wake Hali ambayo imeona faida yake na kutoa wito kwa wazazi ndani na nje ya nchi kuleta watoto kwenye shule hiyo .
Alisema kuwa kupitia maadhimisho ya miaka 30 ya shule hiyo wametoa ofa la punguzo la ada na unalipa kwa mafungu ili kulahisisha wazazi wamudu kulipa ada hiyo iliyopunguzwa kwa asilimia 50 kwani kama tunaweza tumia fedha nyingi kwenye mengine kwanini usiweze kutumia hayo katika kumpa elimu Bora mwanao.
“Elimu atakayopata Iringa International School itamfanya mtoto aweze kujitegemea kutokana na ubora wake hivyo wazazi walete watoto wao wasiangalie Bora shule ila ubora wa elimu inayotolewa hapo inamwezesha mtoto kuishi popote duniani”alisema