Na John Walter -Babati
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameuagiza uongozi wa kijiji cha Galapo kuwalipa akina mama wanaojishughulisha na upondaji wa kokoto fedha wanazodai ifikapo siku ya Jumatatu Februari 26,2024.
Kina mama hao wamemwambia mkuu wa wilaya kwamba walifanya kazi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Galapo ambapo mpaka sasa hawajalipwa fedha wanazodai zaidi ya shilingi Milioni moja.
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameendelea na ziara ya kikazi katika Kata za wilaya hiyo kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Akiwa kata ya Galapo, Twange amewataka wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji kuwahudumia wananchi kwa mujibu wa utaratibu ili kuepuka kero na migogoro na hatimaye kuwa na Maendeleo.
Katika ziara yake mkuu wa wilaya ameambatana na taasisi za serikali na watalaamu wengine ili kujibu kero husika.