ARUSHA: Watu 15 wamefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Lori la Mizigo (Semi Trailer) na magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la Ngaramtoni, Wilayani Arumeru, Februari 24, 2024, ambapo Jeshi la Polisi limesema chanzo cha ajali bado hakijafahamika lakini taarifa za awali zinaonesha Lori lilipoteza uelekeo
Kwa mujibuwa taarifa za mashuhuda, Lori hilo aina ya Scania lenye namba za Usajili ZF 6778 lilikuwa likionesha ishara Taa za Hatari likiwa katika mwendo mkali na baadaye kuyagonga magari matatu ambayo ni Basi dogo la Abiria (Hiace), Basi la Shule ya New Vision lililokuwa na Watumishi wa Shule na Gari lingine dogo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema kuna majeruhi kadhaa ambao wapo katika hali mbaya, pia amewataka Wananchi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kutambua Miili ya waliofariki pamoja na majeruhi katika ajali hiyo
Chanzo Jamii Forum.