Dar es Salaam, Tanzania – Februari 24, 2024
Samsung Electronics Tanzania na Tigo Tanzania wameungana kutangaza upatikanaji wa toleo jipya la Galaxy S24. Kupitia ushirikiano huu, wateja wataweza kufurahia uzoefu bora wa kidigitali na mtandao wa 5G wa Tigo, ambao ni wa kasi zaidi nchini. Pia, Samsung Galaxy S24 itakuja na 96GB ya data ya intaneti za BURE kwa mwaka mzima mteja anunuapo kutoka katika duka lolote la Tigo nchini kote.
Mkurugenzi wa Tigo – Kaskazini, Henry Kinabo alisema, “Kwa ushirikiano na Samsung, ushirikiano wetu katika kutambulisha simu ya Galaxy S24 unathibitisha dhamira yetu ya kutoa vifaa vya hali ya juu kwa wateja wetu, kwa kujumuisha uwezo wa mtandao wa 4G+ na 5G. Tigo, tunaongoza mapinduzi ya kidigitali nchini Tanzania, tukitambua kuwa uongozi endelevu katika uwanja huu unategemea uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya mawasiliano. Tangu mwaka 2022, tumewekeza zaidi ya shilingi trilioni moja za Kitanzania, lengo letu ni kufikia wigo wa 4G kote nchini na kutekeleza 5G katika vituo vikuu vya mijini ifikapo mwisho wa 2024.”
Ni muhimu kufahamu kuwa, uwekezaji wa Tigo katika kuboresha miundombinu yake ya mtandao umepata kutambuliwa kimataifa, ambapo Ookla imethibitisha Tigo kuwa mtandao wa kasi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2023. Aidha, katika ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa robo ya nne ya mwaka 2023, Tigo ilishika nafasi ya kwanza kwa ubora wa huduma. Hii inamaanisha kuwa, wateja wetu wanaonunua simu mbalimbali za Galaxy S24 wanaweza kufurahia huduma bora wakati huo huo wakinufaika na faida za mtandao bora kote nchini ili kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.” Kinabo alisisitiza.
Ujio wa Galaxy S24 umepokelewa vizuri na wateja wa Samsung huku ongezeko la oda ya simu hizi ikiwa ni mara mbili zaidi kulinganisha na toleo lililotangulia. Zaidi ya asilimia 69 ya watumiaji nchini wameonekana wakichagua kutaka kutumia toleo la kisasa zaidi la Galaxy S24 Ultra.
Teknolojia ya AI katika simu za Galaxy S24 inaleta chachu katika ubunifu na matumizi, ikisaidia kubadilisha jinsi watu wanavyowasiliana na dunia. Huduma kama vile Live Translate na Chat Assist zinawezesha mawasiliano bila vikwazo, na utafutaji wa habari unaboreshwa kupitia Circle to Search na Google. ProVisual Engine ambayo ni zana ya kamera zinazoendeshwa na teknolojia hii zinaongeza uhuru wa ubunifu na umahiri wa upigaji na uhariri wa picha.
Akizungumza wakati uzinduzi wa ushirikiano huu, kiongozi wa biashara za kampuni ya Samsung Electronics nchini Tanzania, Manish Jangra alisema kuzinduliwa kwa aina mbalimbazi za simu za Galaxy S24 kunaonyesha hatua ya awali ya kampuni kuanzisha enzi mpya ya simu za AI ambazo ni zaidi ya simu janja zilizopo kwenye soko kwa sasa.
“Galaxy S24 zimetengenezwa kuwa na vionjo ambavyo vitakuwa ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku, na Galaxy AI itabadilisha mitindo ya maisha ya watu duniani. Tuna shauku kubwa ya kuona jinsi watumiaji wetu watavyotumia simu hii kuimarisha maisha yao ya kila siku na kufungua fursa mpya na uwezekano usio na mwisho,” aliongeza
Simu mbalimbali za Galaxy S24 sasa zinapatikana kwa bei zilizopangwa kulingana na aina ya simu; S24 Ultra 12+512 GB itauzwa kwa bei ya reja reja kwa Tzs4,321,000, S24 Ultra 12+ 256 GB kwa Tzs3,961,000, S24+ (pamoja) 12+512 GB kwa reja reja kwa Tzs3,384,000, S24 ikiwa na 12+256 GB inauzwa kwa reja reja Tzs3,024,000, S24 Base 8+256 GB rejareja kwa Tzs2,661,000 na S24 Base 8+ 128 GB ikiuzwa kwa reja reja Tzs2,482,000.
Aina mbalimbali za simu za Galaxy S24 ambazo zimezinduliwa hivi karibuni zitakuwa zinapatikana katika maduka yote ya Samsung na Tigo nchini.