Ikiwa imebakia siku moja kufanyika kwa mbio za kimataifa za Kilimanjaro (Kilimanjaro International Marathon 2024) Timu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki -Nje Jogging – imeendelea na maandalizi ya kushiriki mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 25 Februari 2024 Moshi, Kilimanjaro.
Wanariadha hao wameweka kambi ya siku tatu mjini Moshi wakijifua na hatua za maandalizi ya mbio hizo. Kadhalika, Makatibu Wakuu wa Wizara wanatarajiwa kuungana na timu hiyo katika mbio hizo kesho.
Viongozi hao ni Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Said Shaibu Mussa.
Mbio za Kilimanjaro International Marathon 2024 zitafanyika katika Chuo cha Usharika Moshi (MoCU) ambapo zimeandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon na kuratibiwa kitaifa na Kampuni ya Executive Solutions.