Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga akizungumza katika hafla ya utiaji sain9 mkataba wa huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kwa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Mkongo wa Burundi- Burundi Backbone System.
………………………….
Burundi Backbone System- BBS ni moja ya wateja wa muda mrefu wa shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na shirika hilo linajivunia uhusiano uliopo tangu mwaka 2019, wakati lilipoingia mkataba ya lipoingia na Burundi Backbone System.
Mkataba wa kwanza ulikuwa ni kutoa huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kwa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Mkongo wa Burundi- Burundi Backbone System kupitia eneo la Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi katika Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera na Manyovu kwa upande wa Kigoma.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa kuongeza huduma ya kuwapatia huduma ya mkongo wa Taifa wa Mawasiliano miaka 5 zaidi.
Mhandisi Peter Ulanga amesema hayo baada ya matokeo mazuri ya huduma za Mkongo wa Taifa, jirani zetu Serikali ya Burundi kupitia Burundi Backbone System imekubali kuongeza huduma kutoka kwenye Mkongo wa Taifa wa mawasiliano, kwa Mkataba wa kibiashara wa Miaka Tano(5) wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.3/- sawa Shilingi za Kitanzania Bilioni 8.3/-.
Shirika la Mawasiliano Tanzania liko tayari kutoa huduma bora kwa Burundi kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa kibiashara. Tunaamini ushirikiano huu utaimarisha uhusiano wa kindugu kati ya nchi zetu na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamiii kwa wananchi wa Tanzania na Burundi.
“Tunafurahi sana kuona Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ukiendelea kutumika kwa mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Ubora wa huduma na gharama nafuu za mkongo huu vimetupa motisha ya kuendelea kuwekeza katika miundombinu yake ili iweze kuleta tija zaidi na kuchochea shughuli za maendeleo katika nchi zetu za Afrika,” amesema Mhandisi Peter Ulanga
Amesema mapema mwaka jana 2023, shirika lilifanikiwa kusaini Mkataba wa kibiashara wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Tanzania na Mkongo wa Taifa wa Uganda kwa kushirikiana na Mamlaka ya Taifa ya Teknolojia ya Habari ya Uganda (NITA-U). Pia, 4 lilifanikiwa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Tanzania na Mkongo wa Taifa wa Malawi kupitia Shirika la Umeme la Malawi (ESCOM).
Ameongeza kuwa hadi sasa, tumefanikiwa kuunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, na Zambia. Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeishafika Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji, na juhudi za dhati zinaendelea za kuunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utekelezaji wake unaendelea.
Shirika linaendelea kusimiamia ujenzi wa miradi ya upanuzi wa Mkongo wa Taifa
kikamilifu na matarajio yetu miradi hii itakamilika haraka. Miradi hiyo pamoja na Awamu ya Kwanza yenye Km 4,442 ambayo itafikia wilaya 22, Awamu ya Pili yenye Km 1,520 ambayo itafikia wilaya 32 na Upanuzi wa Njia Kuu kutoka 800Gbps hadi 2Tbps kwa mizunguko ya Kaskazini na Magharibi; na Awamu ya Tatu yenye Km 928 ambayo itafikia Wilaya 5 vinajengwa pamoja na upanuzi wa hadi 2Tbps kwenye mradi wa upanuzi wa ndani kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mhandisi Peter Ulanga amempongeza Waziri wa Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye(Mb), kwa kukubali kushuhudia tukio hili muhimu na la kimkakati na Mtendaji Mkuu wa BBS, Bw. Jeremie Diomede Hageringwe, na timu yake yote kwa kuchagua kutumia huduma za NICTBB.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Zuhura Sinare katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga wakiwa katika hafla hiyo.
Picha zikionesha Voingozi na wadau mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.