Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizindua na kumkabidhi nyumba aliyomjengea Bw. Hosea Kalemale Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya ambaye ni mlemavu wa macho leo tarehe 23 Februari, 2024.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimuongoza kutembea Bw. Hosea Kalemale (katikati) Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya ambaye ni mlemavu wa macho kuelekea kwenye nyumba aliyomjengea leo tarehe 23 Februari, 2024. (kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya Mjini Bw. Clement Mwandemba)
Muonekano wa nyumba aliyoijenga Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa ajili ya makazi ya Bw. Hosea Kalemale Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya ambaye ni mlemavu wa macho leo tarehe 23 Februari, 2024.
………………
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amezindua na kumkabidhi nyumba aliyomkarabatia Bw. Hosea Kalemale Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya ambaye ni mlemavu wa macho leo tarehe 23 Februari, 2024.
Dkt. Tulia amemkabidhi Hosea nyumba hiyo yenye vyumba viwili vya kulala, sebule pamoja na choo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa siku kadhaa mara baada ya kuombwa hitaji hilo.