Pombe na matusi vimeelezwa kuwa chanzo cha ukatili wa jinsia Kwa wanawake katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Akizungumza wakati mkutano wa wahudumu wa bar,Mkaguzi msaidizi wa polisi Asha Mponda na mkuu wa dawati jinsia na watoto wilaya ya Nachingwea alisema kuwa kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zinatokana unywaji wa pombe kupitia kiasi.
Mponda alisema kuwa wanawake wengi wilaya ya Nachingwea wanapokea vipigo kutoka kwa wanaume kutokana na matusi wanayoyatoa wanaume wakiwa wamelewa.
Nao wahudumu wa bar katika wilaya ya Nachingwea wamesema mabosi zao,polisi na wanajeshi wamekuwa wanawafanyia ukatili wa jinsia hadharani hivyo wanaomba serikali ya wilaya kuingilia kati suala hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amesema hawatakubali vitendo hivyo kuendelea katika wilaya hiyo huku dhamira kubwa ikiwa kuifungua wilaya kiuchumi.
Baadhi ya wameriki wa bar wilaya ya Nachingwea wamesema kuwa hakuna muajiri anayenyanyasa wahudumu ila wahudumu wanashindwa kufaata taratibu za kazi