NA JOHN BUKUKU- DAR ES SALAAM
Kutokana na kuwepo kwa changamoto kwa baadhi ya wadau wa maendeleo wanapoleta fedha nchini zinaenda kufanya shughuli ambazo hazigusi wakulima kama vile semina na Warsha ma Makongamano Serikali ya Tanzania na Norway zimesaini mikataba ambao umefanywa marekebisho na kutatua changamoto hiyo ambapo sasa fedha hizo za wadau zitaemda kugusa maemdeleo ya kisekta miradi ya kiutafiti moja kwa moja.
Hayo yamebainishwa leo alhamisi Feburuari 22, 2024 na Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe wakati akijibu maswali katika mkutano wa wahariri ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan katika nchi za Italia,Norway na Ethiopia.
Amesema kama Wizara waliamua kuongea na wadau wa maendeleo wanapoleta fedha za maendeleo lazima zitumike kutatua changamoto za msingi za Sekta ya Kilimo.
“Naishukuru sana Serikali ya Norway kukubali kusaini fedha zao za maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano za kusaidia sekta za kilimo ambazo zitaelekezwa katika maeneo ambayo Serikali ya Tanzania inaamini ni maeneo ya msingi”, amesema Bashe
Aidha, ameeleza kuwa wamesaini makubaliano ya shilingi Bilioni mbili kutoka taasisi ya utafiti ya Norway kwa ajili ya kuisaidia taasisi ya utafiti ya kilimo Tanzania (TARI) ambapo fedha hizo zitaenda kwenye suala la kupima afya ya udongo.
Amesema wamekuwa wakihamasisha wakulima kutumia mbolea lakini kuna maeneo ambayo tumeyafanyia utafiti na kukuta tindikali ya aridhi iko juu ambapo ukipeleka mbolea ya kiwandani unaenda kuongeza tindikali zaidi kwenye ardhi.
“Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya Utafiti wa kupima afya za udongo na tunapozungumzia usalama wa chakula ni mjumuisho wa afya ya udongo, upatikanaji wa mbegu pamoja na shughuli zote za utafiti”, amesema Bashe
Ameeleza kuwa mwaka 2022 waliruhusu wakulima kuuza mazao yao popote jamba ambalo lilitea shida kwenye upatikanaji wa chakula nchini kutokana na bei kuwa juu hivyo Serikali iliamua kuchukua hatua ya kutoa ruzuku kwa wakulima ili wapate hamasa ya kuingia shambani.
“Mwaka ulioisha wa chakula uzalishaji ulikuwa tani milino 17 leo mwaka mzima wa Kilimo umeisha uzalishaji umefikia tani milioni 20, Serikali ilipotoa ruzuku uzalishaji uliongezeka hususani mahindi sokoni bei zimeshuka ambapo siri ya kushuka kwa bei ni pamoja na kupunguza ghrama za uzalishaji na kuhakikisha mkulima hapati hasara kwenye zao analozalisha”,
Akizungumza sula la upelekaji wa mazao nje ya nchi Waziri Bashe amesema wasiporuhusu mazao kwenda nje watakuwa wamezuia shughuli za watu za uzalishaji ila wanachotakiwa kufanya nikuongeza tija kwenye kilimo kwa kuendelea kutoa ruzuku ya mbegu,mbolea ili wakulima wazalishe kwa wingi.
Akijibu swali la upandishaji wa bei za mazao kiholela Waziri Bashe amesema Serikali imeanza utekelezaji wa sheria ya mwaka 2009 ya mamlaka ya kusimamia mazao yasiyokuwa na kodi itakayosaidia kuwakamata wafanyabiashara wanaopadisha bei kiholela.