Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Rufaa (Mstaafu) Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa
Uchaguzi ambao wanakwenda kusimamia uchaguzi mdogo katika Kata 23 za Tanzania Bara
yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Morogoro. Uchaguzi unataraji kufanyika Machi
20,2024.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamaliwatu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Silas Marwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Hamlmashauri ya Mji wa Kibaha, Eng. Mshamu Ally Munde akizungumza kwa niaba ya washiriki.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mdogo wa udiwani kwa Kata 23 za Tanzania bara yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa siku tatu. Uchaguzi unataraji kufanyika Machi 20,2024.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mdogo wa udiwani kwa Kata 23 za Tanzania bara yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa siku tatu. Uchaguzi unataraji kufanyika Machi 20,2024.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mdogo wa udiwani kwa Kata 23 za Tanzania bara yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa siku tatu. Uchaguzi unataraji kufanyika Machi 20,2024.
wa kata 23 za Tanzania Bara kukamilisha maandalizi muhimu kwa wakati ili kuwezesha uchaguzi huo kufanyika kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Rufaa (Mstaafu) Mhe. Mbarouk
Salim Mbarouk leo tarehe 22 Machi, 2024 wakati akifunga mafunzo kwa watendaji hoa yalifanyika mkoani Morogoro.
Uchaguzi
huo utafanyika tarehe 20 Machi, 2024 ambapo fomu za uteuzi zitatolewa kuanzia tarehe 27 Februari, 2024 hadi tarehe 04 Machi, 2024, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 04 Machi, 2024 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia
tarehe 05 hadi 19 Machi, 2024.
“Mnatakiwa kukamilisha mambo yote muhimu yanayotakiwa kwenye mchakato wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kubandika
matangazo na mabango mbalimbali ya kisheria kuhusiana na uchaguzi kwa mujibu wa maelekezo,” amesema Jaji Mbarouk.
Aliwakumbusha
watendaji hao kuwa wapo wadau mbalimbali wa uchaguzi kama vile vyama vya siasa, wananchi na watazamaji ambao wanafuatilia uendeshwaji wa uchaguzi na kiwango
cha uzingatiwaji wa sheria zinazohusiana na uchaguzi. Hivyo, ni muhimu wakatekeleza kila hatua na kila jambo linalotakiwa kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi.
“Jukumu lililopo mbele yetu ni kubwa na muhimu na linahitaji umakini, na kujitoa, na hasa baada ya kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha uchaguzi wa tarehe 20
Machi, 2024,” Jaji Mbarouk amewaambia watendaji hao.
Amesisitiza
juu ya umuhimu wa watendaji hao kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, Sheria na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki.
Kata zitakazofanya uchaguzi huo mdogo ni Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa
(Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji
Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).
Nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma), Busegwe
(Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya
Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).