Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (katikati) akiwa katika picha pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy, Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Festo Sanga wakati akikata utepe katika uzinduzi wa vitendea kazi vya doria za misituni vya TFS iliyofanyika leo tarehe 20/2/2024 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza leo tarehe 20/2/2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya doria za misituni vya TFS.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza leo tarehe 20/2/2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya doria za misituni vya TFS.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy akizungumza leo tarehe 20/2/2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya doria za misituni vya TFS.
Vitendea kazi vya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambavyo vimezinduliwa leo tarehe 20/2/2024 Jijini Dar es Salaam.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki amezindua vitendea kazi vya doria za misituni vya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambavyo ni magari manne ikiwemo land Cruiser mbili, magari mawili Maalamu ya doria katika mazingira mzituni, pikipiki 39 kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika shughuli mbalimbali ikiwemo ulinzi na usimamizi wa misitu.
Akizungumza leo February 20, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa vitendea kazi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, amesema kuwa anaamini vitendea kazi hivyo magari na pikipiki zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa na kuleta mabadiliko katika ulinzi na usimamizi misitu nchini.
“Tunaamini pikipiki hizi zitakwenda kusaidia usimamizi wa misitu wa nyuki, mashamba ya miti, vituo vya kukusanya mbegu za miti pamoja na mashamba ya ufugaji wa nyuki” amesema Mhe. Kairuki.
Mhe. Kairuki amesema kuwa TFS inawajibu mkubwa wa kuweka jitihadi katika ulinzi wa rasilimali zilizopo pamoja na kuvutia uwekezaji wa kimkakati ili kupata viwanda vya kuchakata mazao ya misitu pamoja na nyuki.
Amesema kuwa rasilimali za misitu na nyuki zinamchango mkubwa katika uchumi ambapo inachangia wastani wa asilimia 3.5 katika pato la Taifa, huku asilimia 17 zikitoka katika sekta ya utalii.
Mhe. Kairuki amewapongeza TFS kwa kuboresha utendaji kwa kununua vitendea kazi ambavyo vina uwezo mkubwa wa kutoa huduma ya doria katika mazingira magumu ya misitu, huku akisisiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo, amesema kuwa wameendelea kuboresha mazingira ya kazi na vitendea kazi ikiwemo kujenga vituo vya ulinzi wa misitu pamoja na ununuzi wa vyombo usafiri na mitambo.
Prof. Silayo amesema kuwa
magari mawili maalamu kwa ajili ya doria katika mazingira msituni yana thamani ya shilingi milioni 773, huku pikiki 39 zikiwa na thamani ya shillingi milioni 452.9 ambazo zitatumika katika usimamizi wa rasilimali za misitu katika maeneo mbalimbali nchini.
Amefafanua kuwa pia kuna magari mawili aina Land Cruiser hard Top ambayo yamenunhliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania kwa ajili ya matumizi ya TFS yenye thamani ya shilingi milioni 337.3.
“TFS inaendelea na jitihada ya kuongeza vitendea kazi, mwaka huu wa fedha tumepanga kununua magari 21, matreta mawili, roli moja, drone mbili kwa ajili ya kufanya doria ya kimkakati zote kwa pamoja zitagharimu shilingi bilioni 6.3” amesema Prof. Silayo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy, amesema kuwa vitendea kazi hivyo vimekuja katika wakati sahihi katika kuleta ufanisi kwani Yana uwezo wa kuingia katika mashamba.
Amewashukuru wadau mbalimbali ikiwemo Wizara na Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kwa kutoa ushirikiano TFS ili hakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa na kuleta tija kwa Taifa.