Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kulia ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Caren Kahangwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Watendaji Waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka kulia, Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi, Bi. Juliana Mkalimoto, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Sarah Kibonde (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, Bw. Thomas Chali wakifuatilia mkutano baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa leo Februari 20, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, Bw. Thomas Chali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma kuhusu hatua za utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, Bw. Thomas Chali(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………
Taasisi za umma zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku kutoka katika Wizara sita zimetekeleza maelekezo ya Serikali ya kuhama kutoka matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa kinara kwa taasisi zake kutekeleza agizo hili la Serikali kwa zaidi ya asilimia 85.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20, 2024 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa maelekezo ya usitishaji wamatumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi za umma.
Amesema lengo la maelekezo hayo ni kupunguza madhara ya kiafya na mazingira yanayosababishwa na kukithiri kwa matumizi ya kuni na mkaa katika jamii zetu na ukataji wa miti kwa ajili ya nishati ya kupikia.
Dkt. Jafo amesisitiza kuwa katazo hilo haliwahusu watumiaji katika ngazi ya kaya na watumiaji wadogo bali limeanza kwa watumiaji wakubwa na Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi hao ili waanze kutumia nishati safi ya kupikia
“Kama nilivyosema awali Taasisi hizo ziko chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,” amesema Dkt. Jafo.
Dkt. Jafo amesema Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 inahimiza umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira ikiwemo rasilimali za misitu, hivyo ili kufikia lengo hilo, Sera inahamasisha matumizi ya nishati mbadala wa kuni na mkaa kwa lengo la kupunguza ukataji miti na uharibifu wa misitu.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazoandaa na kulisha watu zaidi ya mia moja (100) kwa siku, ifikapo Januari, 2024 ambapo katika taarifa yake ya utekelezaji Wizara hizo zimetuma mipango husika ya matumizi ya nishati mbadala na jinsi zitakavyotekeleza agizo hili.
Kwa mujibu wa Dkt. Jafo, katika sekta ya Elimu hadi kufikia Januari 31, mwaka huu jumla ya Vyuo vya Ualimu 30 kati ya 35 sawa na asilimia 85.71 ya lengo, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 51 kati ya 54 sawa na asilimia 94.44 ya lengo, na Vyuo vya Elimu ya Ufundi (VETA) vinane (8) kati ya 36 sawa na asilimia 22.22 vimeshaunganishwa na huduma ya Nishati Mbadala ya Kuni Poa.
Amefafanua kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kuna jumla ya Taasisi 8 ambapo 6 ni vyuo vya maendeleo ya Jamii na taasisi mbili ni vyuo vya maendeleo ya jamii na ufundi. Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Uyole kwa sasa vimeanza kutumia Nishati mbadala sawa na asilimia 25 ya lengo.
Aidha Dkt. Jafo ameeleza kuwa katika Sekta ya Afya hadi kufikia Januari 31 mwaka huu Hospitali tatu (3) ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala (DSM), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma na Kituo cha Afya Sinza (DSM) tayari zimeanza kuzalisha gesi.
Kuhusu taasisi zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Chuo cha Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu na shule ya Polisi Tanzania zinatumia majiko yenye mfumo wa gesi.
Na baadhi ya vyuo ikiwemo Chuo cha Polisi Zanzibar wanatumia gesi na kuni kidogo.“Jeshi la Magereza lina jumla ya Magereza 129, Vyuo vya Magereza vinne (4) na Shule za Sekondari Bwawani.
Kati ya vituo hivyo jumla ya Magereza 76 sawa na asilimia 58.91, Vyuo 3 sawa na asilimia 75 ya vyuo vya magereza, na Sekondari ya Bwawani yameanza kuacha kutumia kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati mbadala ikiwemo gesi asilia” amesema Dkt. Jafo.
Katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Jafo amesema asilimia 90 ya baadhi ya vikosi vinatumia nishati mbadala kama vile gesi wakati huo vikosi vingine vikiwa vimetekeleza kwa kiwango cha wastani kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia gesi.
Aidha Dkt. Jafo amesema katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambayo inamiliki kiwango kikubwa cha shule za Msingi na Sekondari nchini, jumla ya shule 571 za bweni zenye wanafunzi wapatao 156,622.
Kati ya shule hizo za bweni, shule 67 sawa na asilimia 11.73 zimefungwa mifumo ya gesi ambapo shule 60 kati ya hizo zinatumia mufumo ya gesi.
Amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta ipo kwenye maandalizi ya kuunda Timu ya Wataalam itakayoweza kutembelea taasisi husika ili kufuatilia hatua zinazoendelea katika utekelezaji wa katazo hilo na kutoa ushauri wa kitaalam.
Itakumbukwa kuwa tarehe 01 Novemba, 2022, Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ambapo aliekeza kusitisha matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazolisha watu Zaidi 100 kwa siku, ifikapo Januari 31, 2024.