Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewapandisha vyeo jumla ya maofisa wa Polisi 155.
Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi 27 na Makamishna Wasaidizi wa Polisi kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi 128 ambao wamekula kiapo cha Utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na Kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma.
Akitoa nasaha zake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, kupandishwa vyeo kwa maofisa hao kutaongeza chachu ya utendaji kazi, kutenda haki, uadilifu na nidhamu pia wananchi wategemee mabadiliko makubwa ya kiutendaji.
Naye kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu CP Susan Kaganda amesema miongoni mwa waliopandishwa vyeo pia wapo maofisa nane wa kike ambao wamepanda vyeo na kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi
Akizungumza kwa niaba ya waliopandishwa vyeo Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi David Misime amesema kupanda kwao vyeo kutaongeza morali na utimamu zaidi wa akili katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi.