NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa fedha na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 1.7 kwa ajili ya kukabidhiwa washindi watakashinda katika michuano ya kombe la Kibafa Vijana Cup wenye umri chini ya miaka 25.
Michuano hiyo ya fainali ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na mashabiki wa soka inatarajiwa kulindima Februari 21 mwaka huu kwenye uwanja wa Mwendapole mjini kibaha.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mbunge katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Method Mselewa wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika ofisi za Mbunge na kuhudhuliwa na viongozi wa Kibafa na wadau wa soka.
Katibu Mselewa alibainisha kwamba wakati wa mashindano yananza Mbunge aliahidi kuwa mdhamini mkuu wa michuano hiyo na kutoa vifaa mbali mbali kwa ajili ya timu zishiriki.
Mselewa alibainisha kwamba ofisi ya mbunge imeweza kukabidhi zawadi mbali mbali ikiwemo fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya timu itakayoibuka kuwa bingwa.
“Mbunge aliahidii kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu na leo tumekabidhi zawadi hizo kwa viongozi wa Kibafa ambapo milioni moja kwa mshindi wa kwanza laki tano mshindi pili na mshindi wa tatu zawadi ya jezi,”alisema Mselewa.
Aidha aliongeza kuwa mbunge aliamua kusapoti michuano hiyo kwa lengo la kuweza kukuza na kuibua vipaji kwa vijana wa jimbo lake ikiwa pia ni utekelezaji wa ilani ya chama.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kibafa David Mramba amempongeza Kwa dhati kwa kuweza kusapoti mashindano hayo pamoja na kutoa jezi na vifaa Ili kufanikisha ligi hiyo ya vijana.
Pia alifafanua kwamba katika ligi hiyo Mbunge aliweza kutoa jezi 16 pamoja na mipira 20 kwa timu zote 16 ambazo zimeshiriki katika michuano hiyo.
Naye meneja wa mashindano hayo Walter Mwemezi alisema alimpongeza Mbunge huyo kwa kuweza kufanikisha ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa zawadi kwa timu zitakazoshinda.
Pia aliongeza kuwa mashindano hayo yameweza kupewa sapoti kubwa na mbunge kuanzia mwanzo na amekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya michezo.
Kivumbi cha fainali za michuanoo hiyo ambayo ilizishirikisha timu 16 za Jimbo la la Kibaha mjini kinatarajiwa kufikia tamati yake Februari 21 mwaka huu katika viwanja vya mwendapole ambapo itazikutanishw timu ya Umwerani watamenyana na Chestmocker.