Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Ramadhani Msophe akizungumza na wanachama wa Jumuiya Wazazi Kata ya Ukonga akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika leo February 18, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Mbassa akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ukonga akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika leo February 18, 2024 Jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM, Wilaya ya Ilala wakizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ukonga wakiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika leo February 18, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Ukonga wakiwa katika kikao kazi na Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Msophe ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa Jumuiya Wazazi Kata ya Ukonga kuhakikisha wanafanya uchaguzi ili kujaza nafasi ambazo zipo katika matawi jambo ambalo lisaidia kuongeza uhai wa Jumuiya ndani ya Kata hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya leo February 18, 2023, Kamati ya Utekelezaji Wazazi Wilaya ya Ilala chini ya uongozi wake Mwenyekiti Comred Msophe kufanya ziara Kata ya Ukonga kwa ajili ya kukagua uhai wa Jumuiya katika Kata hiyo.
Akizungumza kwenye Kikao kazi na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ukonga Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Comred Msophe, amesema kuwa Kata ya Ukonga inamapungufu ya kiutendaji, huku akiwasihi uongozi wa wazazi wa Kata hiyo kufanya vikao na matawi saba ili kutatua changamoto zilizopo.
Comred Msophe amesema amesisitiza umuhimu wa Jumuiya ya wazazi kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano jambo ambalo lisaidia kuongeza uhai wa Jumuiya pamoja na kuhakikisha Chama Cha CCM kinashika Dola katika uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu.
Aidha wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi Wilaya kila mmoja alitoa maelekezo ya kuijenga Kata ya Ukonga, huku wakisisitiza kwa pamoja Katibu wa Kata hiyo asimamie vikao pamoja na kufikisha muhtasari Wilayani.
Naye Katibu wa Wazazi Wilaya ya Ilala Mtiti Jirabi amewataka Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi Matawi na Kata kushikamana na kuwa kitu kimoja na kuhakikisha wanakutana mara kwa mara kuijenga Jumuiya.
Katibu huyo amesema kuwa makatibu wa Jumuiya ya Wazazi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kusoma kanuni za Jumuiya ya Wazazi pamoja na miongozo mbalimbali ya Jumuiya na Chama ili kufanya kazi kwa uweledi.