Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Ramadhani Msophe akizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kata ya Kinyerezi akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika February 17, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Mbassa akizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kata ya Kinyerezi akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika February 17, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM, Wilaya ya Ilala wakizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kata ya Kinyerezi wakiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya iliyofanyika February 17, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kinyerezi Sharifa Mkadar akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa majukumu Jumuiya kwa kamati ya utekelezaji Wilaya ya Ilala.
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kinyerezi wakiwa katika kikao kazi na Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala leo February 17, 2024 wamefanya ziara katika Kata ya Kinyerezi kwa ajili ya kukagua uhai wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata hiyo.
Akiwa ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya utekelezaji Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Ramadhani Msophe amekutana na wanachama wa matawi 8 na kufanya ukaguzi wa kamati za utekelezaji matawi kama zimetimia kwa idadi ya Wajumbe kupitia Kanuni ya Jumuiya ya Wazazi.
Ameeleza kuwa kamati ya utekelezaji Wazazi Wilaya imepokea barua kutoka ngazi ya Mkoa kuja Kata ya Kinyerezi kukagua Uhai wa Jumuiya kupitia Matokeo ya ziara ya Kamati ya Utekelezaji Wazazi Mkoa wa Dar-es-Salaam chini ya Mwenyekiti wake Comred Bi-Khadija Ally Said.
Comred Msophe amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mahusiano kati ya Jumuiya ya Wazazi na Chama ngazi ya Matawi na Kata.
Aidha ameeleza kuwa ni muhimu kukaa vikao kwa mujibu wa Kanuni kwenye matawi na Kata ili uleta ufanisi katika utekelezaji.
Ametoa maelekezo kwa kamati ya utekelezaji kuhakikisha vikao vinakalika kwa wakati na makatibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), matawi ni Wajumbe halali wa kamati za utekelezaji matawi.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Mbassa Jirabi amewataka Wanachama wote wa Jumuiya Kufuatilia Taratibu za Kujaza Nafasi za uongozi Mahala penye Magepu ya Uongozi na Ujumbe wa Kamati za Utekelezaji.
Aidha amewataka Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi Matawi kuimarisha Jumuiya ya Wazazi Kiutendaji kwa kuingiza Wanachama kwa Wingi ili kuleta Uwiano mzuri na Chama cha Mapinduzi ccm katika Matawi.
Comred Mtiti amesisitiza Wanachama Kujiandikisha kwenye mfumo wa TEHAMA ili kujuwa idadi kamili ya Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi waliojisajili Electronic Kadi.
Ametoa maagizo kwa wanachama wote na wajumbe wa Kamati za utekelezaji kununua kanuni kwa Tsh 5000/= ili ziwasaidie kujuwa majukumu ya Jumuiya ya Wazazi pamoja na utaratibu wa kufanya vikoa.