Hayo yamesemwa na Meneja wa Programs wa Jamii Forums, Ziada Seukindo wakati akizungumza baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wadau wa Kidigitali ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Jamii Forums kupitia Muunganiko wa Taasisi 24 Zinazofanya Utetezi wa Haki za Kidigitali (Digital Rights Coalition) kwenye Mkutano uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam,
Seukindo amesema mkutano huo umeshirikisha Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kushirikishana changamoto za Teknolojia na jinsi ya kuzipatia utatuzi, ambapo baadhi ya masuala yaliyozungumzwa ni Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Ulinzi wa Faragha pamoja na Maendeleo ya Teknolojia.
Amesema Wadau wanahitaji kupata ushirikishwaji wenye tija badala ya Serikali kufanya maamuzi yenyewe.
Amesema “Tuna wataalam mbalimbali wenye uelewa na wanaoweza kutoa maoni ya kuboresha ‘Digital Space’ ya ndani ya nchi, hivyo tumeshauri Serikali iendelee kutusikiliza na wao imeonesha muitikio chanya kwa kitendo cha kushiriki katika mkutano wetu.”
Ameongeza Mkutano huo umefanyika wakati wa wiki ya Tukio lililondaliwa na Kampuni ya Vodacom likifahamika Kwa jina la Future Ready Summit.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA katika Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari,Mohamed Abdi Mashaka ambaye ni ameahiriki mkutano huo na kusema ushiriki wa Serikali katika Mkutano wa aina hiyo unaendelea kuonesha utayari wa mamlaka kushirikiana na Wadau kuifanya Digitali kuwa katika mikono salama.
“Tumepata nafasi ya kujifunza na kuchukua maoni mengi ili kuweka mazingira wezeshi kwa mfumo mzima na kutumia teknolojia zinazoibukia.
“Mikutano ya aina hii inasaidia kuonesha mwelekeo wa Nchi, ndio maana tunashirikiana na sekta binafsi ili kuifanya jamii kuwa na mwamko wa masuala ya Digitali.”