Na John Bukuku, Zanzibar
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa wito kwa wananchi hususani wanaotumia huduma ndogo za fedha wanapoenda kuchukua mikopo kwa watoa huduma wajiridhishe kwanza kama wamesajiliwa au kupewa leseni.
Wito huo umetolewa leo Februari 16, 2024 na Afisa Mkuu Mwandamizi Kurugenzi ya usimamizi wa huduma ndogo za fedha kutoka BoT Deogratius Mnyamani wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya waandishi wa habari na wahariri inayofanyika katika ofisi za makao makuu ndogo ya Benki hiyo mjini Zanzibar.
Amesema watumiaji wa huduma ndogo za fedha wanatakiwa kusoma vigezo na mashariti nakuyaelewa ili waone kama wataweza kuyatimiza sanjari na kuchukua nakara ya mkataba iliosainiwa ambayo itawasaidia endapo itatokea changamoto yoyote kati yao na watoa huduma.
Ameeleza kuwa kwenye suala la uchukuaji wa mikopo huwa wanawahimiza watanzania kuwa na malengo mahususi ya uchukuaji wa mikopo.
“Tumeona kumekuwepo na malalamiko yanayotoka kwa baadhi ya watu ambao wameathirika na mikopo na malalamiko hayo yanatokana na uchukuaji wa mikopo usiokuwa rasmi,mtu anachukua mkopo bila malengo au shughuli itakayokwenda kuzalisha ili arejeshe mkopo bila vizuri”, amesema
Pia nidhamu ya ulipaji nayo siyo nzuri watu wengi wanachukua mikopo bila kusoma vigezo na mashariti yanayoambatana na mikopo kwenye Kila mkopo kuna riba, ada,tozo na mashariti ya urejeshaji.
“Kunaumuhimu mkubwa sana kwa watanzania kukopa kwenye taasisi zilizopewa leseni na Benki kuu na kama ni sacoss ziwe zimepata leseni kutoka tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.
Amesema kwa suala zima la ufuatiliaji wa sheria na adhabu ambazo zingeweza kutolewa kwa mtoa huduma ambaye hafuati taratibu na kanuni Gavana wa Benki anaweza kusitisha shughuli zote za ukopeshwaji na uwekezaji kwa taasisi ya kifedha endapo ulitonekana imekiuka sheria kanuni za uendesjaji.
Aidha, amesema wanaangalia suala zima la ufuatiliaji wa mikopo kutokana na mikopo hiyo inavyofuatiliwa kwa meseji za vitisho na kejeli hivyo BoT itakaa na wadau mbalimbali wa Tehama,makampuni ya simu ili kuona namna gani suala hili litatolewa muongozo.