Kaimu Mkurugenzi mkuu mfuko wa huduma za Afya ZHSF Yaasin Ameir Juma akifungua warsha ya kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza kwa usajili wa wafanyakazi wa sekta hiyo,huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa bodi mfuko wa huduma za Afya ZHSF Mbarouk Omar Mohammed akizungumzia umuhimu wa kuwa mwanachama wa mfuko huo katika warsha kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza kwa usajili wa wafanyakazi wa sekta hiyo, huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Unguja.
Mkuu wa usajili ZHSF Ali Idrissa Abeid akiwasilisha utaratibu wa usajili kwa sekta binafsi katika warsha ya kuwajengea uelewa waajiri wa sekta hizo juu ya kuanza kwa usajili wa wafanyakazi wao huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Unguja.
Afisa usajili wa wanachama Makame Ame Simai akielezea utaratibu wakuwasilisha michango ya wanachama na namna ya kupata huduma, katika warsha kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza kwa usajili wa wafanyakazi wa sekta hiyo, huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Unguja.
………….
Na Takdir Ali, Maelezo.13.02.2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Mbarouk Omar Mohammed amesema afya ni kitu muhimu katika kuwajenga Wafanyakazi kimwili na Kiakili.
Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) Kariakoo wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo kwa Waajiri wa Sekta binafsi kuhusiana na kuanza usajili wa Wafanyakazi wa Taasisi binafsi, utakaoanza tarehe 01 mwezi ujao.
“afya ndio nyenzo muhimu ya utendaji bila ya Afya nzuri, Wafanyakazi hawatoweza kutoa huduma nzuri katika Taasisi zao.” Alisema mwenyekiti huyo
Aidha amesema Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Wananchi wote wanapata huduma za afya hivyo amewataka Waajiri hao kushirikiana na ZHSF ili kurahisissha zoezi la usajaili na kuweza kutoa huduma bora kwa Wafanyakazi wao.
“Mzigo wa kutoa huduma za Afya ni Mzito ndio Serikali ikaamua kuweka mkakati wa kuboresha huduma za Afya kwa kuanzisha Mfuko huu ili kuona kila mmoja kupata huduma zilizobora” alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo amewataka Waajiri hao kulipa kipao mbele suala la huduma za Afya kwa Wafanyakazi wao kwani kumpatia mfanyakazi huduma za Afya pia ni kuisaidia jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya ya Waajiri Zanzibar (ZANEMA) Salah Salim Salah amesema katika kufanikisha suala hilo wamekuwa wakifanya mazungumzo na Wizara ya Afya mara kwa mara kujadili masuala mbalimbali ya kutoa huduma bora kwa Taasisi binafsi.
Hata hivyo amewataka Waajiri wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali kupitia ZSHF ili zoezi la usajili na kutoa huduma liweze kufanyika kama lilivyopangwa.
Nao Waajiri hao wa Taasisi binafsi wameiomba ZHSF kuimarisha utoaji wa huduma kwa Wanachama wao ikiwemo Majengo,Matibabu na Vipimo ili waweze kupata huduma nzuri na za kuridhisha.
Hata hivyo Wameiomba ZHSf kufanya kazi kwa uadilifu na uwazi ili malengo ya Serikali yaweze kufikiwa.