Bao la kiungo Msenegal, Babacar Sarr dakika ya 81 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 33 na kupanda nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Azam FC baada ya wote kucheza mechi 14 na wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 40 za mechi 15.
Kwa upande wao Geita Gold baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 16 za mechi 14 nafasi ya 10.