RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufunga Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-2-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi maalum Dr. Zahra Khan kutoka Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kwa kujibu vizuri maswali wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, wakati wa ufungaji wa mkutano huo uliyofanyika leo 10-2-2024, na (kulia kwake) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Bi.Asha Ressa Izina, wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-2-2024 na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Prof Dr.Ali Civelek wa Chuo Kikuu cha Istanbul Aydin Turkey, aliyemsomesha wakati akichukua mafunzo ya udaktari Nchini Uturuki, baada ya ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 10-2-2024.(Picha na Ikulu)
………………………….
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Taasisi ya JKCI kwa kuanzisha kitengo cha kuhudumia magonjwa ya moyo Zanzibar katika Hospitali ya Mkoa Lumumba.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati akifunga kongamano hilo la Wataalamu wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo liloandaliwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI na Wizara ya Afya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport lililowashirikisha Wataalamu wa Afya ndani na nje ya nchini tarehe: 10 Februari 2024.
Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali kuwekeza katika vifaa vyote vya matibabu ya Moyo Zanzibar .
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameagiza Wizara ya Afya Zanzibar kuanza haraka majadiliano na Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI ili huduma za upasuaji wa moyo zianze kutolewa Zanzibar kipindi kifupi kijacho.
Rais Dk. Mwinyi pia amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatenga rasilimali zilizopo ili kuendeleza juhudi za utafiti, kinga na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha huduma za Afya kwa kutoa matibabu ya magonjwa ya moyo na kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza wananchi kutumia vyakula vinavyoshauriwa na wataalamu pamoja na kufanya mazoezi.