Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba akizungumza na na wenyeviti,Madiwani na watendaji wa Wilaya hiyo katika kikao cha kutoa Tathmini ya Kampeni ya “KAU-SAPEU” kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo imefanyika katika Ukumbi wa NIT.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba akiwasikiliza kwa makini wadau wa Mazingira ambao walikuwa wanaeleza ushiriki wao katika kampeni ya KAU-SAPEU.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha akizungumza katika kikao cha kutoa Tathmini ya Kampeni ya “KAU-SAPEU” kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo imefanyika katika Ukumbi wa NIT.
Wakazi wa mtaa ambao umekuwa wa mwisho katika suala la usafi wamepatiwa Bendera yanye maandishi ya Balozi wa Uchafu Ubungo.
Baadhi ya wenyeviti,Madiwani,watendani wa Manispaa na wadau wa Mazingira ambao wameshiriki katika kikao cha kutoa Tathmini ya Kampeni ya “KAU-SAPEU” kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo imefanyika katika Ukumbi wa NIT.
……………..…….
NA MUSSA KHALID
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba amewataka wananchi kuhakikisha wanaibeba Kampeni ya Kataa Uchafu,Safisha,Pendezesha Ubungo (KAU-SAPEU) ambayo inatekelezwa kwenye Wilaya hiyo Ili kuepukana na changamoto zinazotokana na Uchafuzi wa Mazingira.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wenyeviti,Madiwani na watendaji wa Wilaya hiyo katika kikao cha kutoa Tathmini ya Kampeni ya “KAU-SAPEU” kwa kipindi cha miezi mitatu sambamba na utoaji wa zawadi kwa mitaa iliyofanya vizuri na iliyofanya vibaya katika Kata zao.
Komba amesema lengo la kampeni hiyo ni kupandikiza misingi na tabia ya wananchi kufanya usafi katika maeneo yao Ili kuepukana na maradhi yanayotokana na Uchafu.
“Amesema kuwa ni lazima Kila mmoja aone fahari kuona Mji unapendeza ,hauna takataka,hauna madampo yaliyokaa holelaholea kwenye maeneo mbalimbali”amesema Dc Komba
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Kampeni hiyo inakwenda sambamba na Utoaji wa zawadi za aina Mbili ikiwemo itakayotolewa kwa muda wa miezi Mitatu mtaa wa kwanza ambao unafanya vizuri wanapata laki sita,mtaa unaofuata laki Nne,na mtaa utakaofata utapata laki tatu.
“Kwa kweli sisi sio wabaguzi kwa kutoa zawadi kwa mitaa ambayo imefanya vizuri hivyo kwa mitaa ambayo itakuwa imekithiri Uchafu tunawatendea haki wataondoka na bendera inayotisha imeandikwa balozi wa Uchafu Ubungo”ameendelea kusema DC Komba
Ameitaja mitaa ambayo inaongoza kwa kwa kutokuwa na mazingira masafi kuwa ni pamoja na Kilimahewa na Kwa Jongo Kata ya Makurumla,Muungano na Midizini iliyopo Kata ya Manzese.
Amesema kukamilika kwa miezi Mitatu leo wanakwenda kuanza Kampeni kwa Awamu ya Pili ambapo atahakikisha anaambatana na mabalozi wa Mazingira kwenye eneo husika ambalo wananchi wametoa taarifa kukithiri kwa Uchafu Mpaka watakaposafirisha.
Awali akizungumza Afisa Mazingira anayeshughulikia Udhibiti wa takangumu na Usafirishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad wakati akielezea namna mchakato wa kampeni ulivyofanyika amesema kwa kushirikiana na wajumbe na mabalozi wa usafi walikuwa wakipita katika maeneo mbalimbali na kubaini ipo mitaa ambayo inatunza mazingira na mingine ni michafu hivyo wakaamua kuja na taratibu za kutoa zawadi
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuanzisha Kampeni hiyo kwani itakwenda kusaidia kupendezesha Manispaa hiyo ya Ubungo.