Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana Msiba wa Waziri Mkuu wa Mstaafu Edward Lowasa, Pole sana kwa wanafamilia,ndugu, jamaa na marafiki kwa kipindi hiki kigumu cha msiba wa mzee wetu.
Edward Lowasa alikuwa mtu aliyempenda Mungu na mwenye upendo na kila mtu hakuwa na majivuno alikuwa mtu mnyenyekevu,wakati mwingine ukimpigia simu anapokea alikuwa hamdharau mtu yoyote nakumbuka hata unapokwenda Ofisini kwake anakupokea hakuwa akikataa wageni alikuwa anamheshimu kila mtu ,rafiki yake akipata matatizo huwa hawezi kumkimbia au kumwaacha na kusema amechafuka bali humuita na kumtia moyo na kumshauri pamoja kumsaidia.
Hakika Taifa limempoteza mtu makini sana hatuna jinsi zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo kwa wakati wa uhai wake jina la Mungu libarikiwe na ampumbuzishe mahala pema peponi Amina.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.