Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amesema si vema kumdhalau mtu kwa sababu wewe unacho na yeye hana kwa sababu huwezi kujua kesho yake ipo aliyopangiwa na Mungu.
“Huwezi kumdharau mtu sababu una cheo ukajiona wewe mkubwa, yawezekana wewe leo hii ukawa mbele na kesho ukarudi nyuma”
“Wanaomdharau Ndugu. Daniel Chongolo niwaambie tu wanajidanganya kwa sababu ni kijana na siku yoyote anaweza kuwa Kiongozi na waliomdharau wakabaki wanajinawanawa tuu”
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi nje ya Ofisi ya Manispaa ya Iringa.