Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametia saini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Namibia nchini, kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Namibia Hayati Dkt. Hage Geingob, kilichotokea tarehe 4 Februari, 2024.
Baada ya kutia saini kitabu, Rais Mstaafu alipata nafasi ya kuzungumza na Balozi wa Namibia nchini, Mheshimiwa Lebbius Tangeni Tobias, pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo ampapo pamoja na mambo mengine, amewapa pole kwa msiba mzito waliopata wa kuondokewa na kiongozi mahiri na mzalendo kwa nchi yake.
Aidha, amemwelezea Hayati Geingob kama rafiki yake wa karibu na kiongozi imara na kuwa Afrika, SADC na Tanzania wamepoteza kiongozi na mdau muhimu.