Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwepo kwa amani katika nchi ya Palestina huku akionyesha matamanio yake ni kuiona nchi hiyo hasa katika ukanda wa gaza wakiendelea kupata huduma muhimu kama kawaida bila kubugudhuwa wala machafuko.
“Tanzania inalaani kuhusu vita vinavyoendelea huko Palestina ambavyo vimesababisha mauaji yasiyo na sababu ya msingi ya watoto wasio na hatia na raia” RAIS SAMIA SULUHU
Akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party), Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesisitiza kuhusu suluhisho la kudumu kati ya Palestina na Israel lakini pia ametoa wito wa kukoma kwa mapigano na kurudisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Gaza.
“Tunasisitiza umuhimu wa kupatikana kwa suluhisho la kudumu na tunaunga mkono suluhisho la mataifa mawili kati ya Palestina na Israel, ikiruhusu wao kuishi pamoja kwa amani na kuheshimiana ndani ya mipaka ya kabla ya mwaka 1967. Pia, tunatoa wito wa kukomeshwa kwa mapigano na kuanzisha tena upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.” RAIS SAMIA SULUHU