Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 baada ya kuwapiga Timu ya Taifa ya Kidemokrasia ya Congo bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali.
Kufatia ushindi huo Wenyeji michuano hiyo Ivory Coast ataminyana na Timu ya Taifa ya Nigeria katika mchezo wa fainali Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 baada Nigeria kuwatoa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika hatua ya nusu fainali.
Ivory Coast walipata bao dakika ya 65 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Sebastién Haller akimpita kipa wa timu pinzani kwa shuti kali.
Ivory Coast imetinga fainali ikiwa timu bora iliyoshika nafasi ya tatu katika hatua ya makundi, na safari yao, ikiwa ni pamoja na kuachana na kocha wao.